Tanzania Safari Channel

1.1 · Android - Bởi TBC3

· 05/05/2020 17:01 (4 năm trước)

Giới Thiệu · Tanzania Safari Channel

Chaneli ya Utalii (Tanzania Safari Channel) ilizinduliwa rasmi na Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 15/12/2018. Lengo la kuanzisha Chaneli hii ni kukuza utalii wa ndani na nje na halikadhalika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa uhifadhi.

Maudhui ya Chaneli hii yanalenga kuangazia maeneo ya uhifadhi kama vile: Wanyama wa porini, Viumbe wa Baharini, Misitu, Fukwe, Miamba na Majabari, Utamaduni, Malikale, Michezo, Kumbi za Mikutano na mengineyo.

Madhumuni ya Chaneli hii ni pamoja na:

i. Kuwawezesha Watanzania kuona na kubaini vivutio mbalimbali vilivyoko katika maeneo yote nchini;

ii. Kuwahamasisha wananchi wajenge utamaduni wa kutembelea maeneo yenye vivutio nchini;

iii. Kutangaza duniani vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii kutoka nje ya Nchi;

iv. Kuieleza na kuikumbusha Dunia kwamba Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro na hata Zanzibar vipo Tanzania;

v. Kuhamasisha wananchi kutunza, kuenzi na kudumisha tamaduni za asili;

vi. Kuangazia na kuibua fursa mbalimbali zilizopo kwenye mnyororo wa biashara katika Sekta ya Utalii; na

vii. Kuyaenzi maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere, aliyoyatoa mwaka 1961, kwamba sisi sote tuna jukumu kubwa la kulinda na kuhifadhi vivutio vya utalii kwa manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo.

Full Specifications · Google Chrome Zing MP3

Phiên bản 1.1
Cập nhật 05/05/2020 (4 năm trước)
Nhà phát triển TBC3
Thể loại Video Software
Hệ điều hành Android
Hệ điều hành cài đặt Android
Yêu cầu Requires Android 4.2 and up
Lượt tải về 51,285

Bình luận